NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, leo amezitembelea ofisi za Global Group ambapo pamoja na kufanya mahojiano kuhusu mafanikio yake katika soka, ametaka mashabiki wa mchezo huo kufurika Uwanja wa Taifa kesho kwa ajili ya mechi itakayokutanisha timu teule yake na ya mwanamuziki maarufu nchini, Alikiba.
Akifanya mahojiano na +255 Global Radio, Samatta alitolea ufafanuzi kwa namna ambavyo alipata wazo la kuanzisha Samakiba Foundation ambayo kesho itakuwa inachezwa kwa msimu wa pili katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo alisema lengo kubwa ni kurudisha kitu kidogo kwa jamii kupitia soka na alimuona Alikiba kama mtu sahihi wa kushirikiana naye.
“Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya watu ambao wana mahitaji kwani pesa zitakazopatikana zitakwenda moja kwa moja kwao, hivyo naomba mashabiki waje kwa wingi ili waweze kutusapoti katika kufanikisha jambo hili,”alisema Samatta.
Amewataja baadhi ya wachezaji ambao wataunda kikosi chake kuwa ni pamoja na Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Kelvin John ‘Mbappe’, Hassan Kessy, Mrisho Ngasa, Athuman Idd ‘Chuji’ na nyota wengine kibao. kutoka Ligi Kuu. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni na kiingilio ni Sh. 2,000 kwa mzunguko.
PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL
The post Samatta Atembelea Global Group, Aomba Mashabiki Wafurike Taifa (Picha +Video) appeared first on Global Publishers.
0 Comments