Faru watano walio kwenye hatari kubwa ya kutoweka wamepokelewa na Rwanda kutoka Ulaya. Kwa mujibu wa Bodi ya maendeleo ya Rwanda faru hao watatunzwa katika mbuga ya taifa ya Akagera, iliyoko mashariki mwa Rwanda.
Hatua hiyo inatokana na jumuiya ya bustani za wanyama ya Ulaya, serikali ya Rwanda na shirika lisilo la kiserikali la African Parks, inayosimamia mbuga ya wanyama ya Akagera pamoja na bodi ya maendeleo ya Rwanda.
Mkuu wa idara ya hifadhi ya Bodi ya Maendeleo ya Rwanda Bw. Eugene Mutangana, amesema faru hao kuhamishiwa Rwanda kutahimiza sekta ya utalii, ambayo huiingizia mapato serikali ya Rwanda.
Wanyama hao walikusanywa mwaka jana kutoka kwenye bustani kadhaa za wanyama kutoka Ulaya kabla ya kusafirishwa kwenda Rwanda.
0 Comments