MFANYABIASHARA maarufu nchini ambaye pia aliwahi kuwa mbunge, Rostam Aziz, ametuma ujumbe kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa ataichangia Klabu ya Yanga kiasi cha Tsh milioni 200.
Hayo yamesemwa leo Jumamosi, Juni 15, 2019 na Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa harambee ya kuichangia Yanga ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
“Nikiwa njiani ninakuja huku Rostam Aziz akanipigia simu akiwa Marekani, amenambia nimsemee, yeye atachangia Milioni 200 kama mchango wake, akaongeza atakapowasili na kukabidhi hiyo pesa atahitaji aonane na mwenyekiti wa timu, Dkt. Msolla na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji, Anthony Mavunde.
Katika hafla hiyo, Waziri Mkuu wa JMT, Kassim Majaliwa ameichangia Yanga shilingi milioni 10, huku Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akichangia Tsh milioni tano. Aidha, na Kampuni ya GSM imetoa mchango wa Tsh milioni 300.
Mbunge wa Iramba Magharibi na mlezi wa klabu ya Singida United, Mwigulu Nchemba, amesema atalipa gharama za usajili wa mchezaji mmoja wa ndani (Mtanzania) kama alivyofanya kwa Feisal Salum ‘Feo Toto.’
Kubwa Kuliko Tamasha la kuichangia Yanga (Sh)
1. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa— Milioni 10
2. Jakaya Kikwete-Milioni 5
3. GSM-Milioni 300
4. Rostam Aziz milioni 200
5. Kamati-Uhamasishaji milioni 50
6. Wabunge mashabiki milioni 40
7. Kamati ya utendaji milioni 50
The post Rostam Awapa Yanga Tsh 200m, GSM Waangusha Tsh 300m – Video appeared first on Global Publishers.
0 Comments