Kampeni ya Matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto 60 kutoka familia zenye maisha duni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda imezidi kugusa Mioyo ya wadau na watu mbalimbali ambapo leo Kampuni ya Ako Group Ltd imeahidi kutoa mchango Shilingi Milioni10 kwaajili ya matibabu ya watoto 5 huku wanachama wa Chama cha Washehereshaji Tanzania wakichangia kiasi Cha Shilingi milioni 3.3 kwaajili ya matibabu kwa watoto wenye tatizo la moyo.

RC Makonda amesema fedha hizo zitawezesha matibabu ya upasuaji wa moyo kwa Watoto 7 ambapo ametoa wito kwa wadau, taasisi na kampuni mbalimbali kusaidia matibabu ili kuokoa maisha yao.

Hayo yamejiri wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Washehereshaji ambapo katika michango hiyo kampuni ya Ako Group Ltd imetoa ahadi ya kusaidia matibabu ya watoto 5 na chama cha washehereshaji kimejitolea kugharamia matibabu kwa watoto 2 na kufanya idadi kuwa watoto7.

Itakumbukwa jumamosi ya juni 22 RC Makonda alitoa ufadhili wa matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto 10 kati ya 60 ikiwa ni mkakati wake wa matibabu ya watoto 10 kila mwezi.