Na Mathew kwembe-Mtwara
Timu ya soka ya wavulana ya mkoa wa Mwanza imeendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya UMITASHUMTA inayofanyika katika viwanja vya chuo cha Ualimu Mtwara ambapo katika mechi iliyochezwa jana ya kundi B linaloundwa na mikoa ya Pwani, Mwanza, Iringa, Lindi na Mtwara iliiadhibu vikali timu ya soka ya mkoa wa Pwani kwa magoli 3-0.
Magoli yote matatu ya Mwanza yalifungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Haroub Juma ambaye ni mwanafunzi wa shule ya academy ya Alliance ya jijini humo.
Huu ni mchezo wa pili kwa timu hiyo ya mwanza kuibuka na ushindi wa kishindo baada ya juzi kuifunga timu ya soka ya wavulana kutoka mkoa wa Mbeya kwa magoli 5-2.
Kufuatia matokeo hayo, timu hiyo imeshinda michezo yake yote miwili ambapo Mshambuliaji wake Haroub Juma ndiye anaongoza kwa kufunga magoli mengi katika michuano hiyo baada ya kufunga magoli matano katika michezo miwili iliyocheza.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, mchezaji Haroub ambaye pia ndiye nahodha wa timu ya soka wavulana Mwanza alisema kuwa timu yake ilistahili ushindi kwani walijiandaa vya kutosha kuikabili timu yoyote watakayopangiwa kucheza nayo.
Naye kocha wa timu hiyo Mwalimu Mathias Wandiba aliipongeza serikali kwa kufanyika kwa mashindano hayo na kuwataka wadau wa michezo nchini hususani TFF kurekebisha kalenda zao ili kwanza wapishe kufanyika kwa mashindano hayo.
“TFF hawana budi kuwasiliana na serikali ambao ndiyo wanaoandaa mashindano ili kutofautisha kalenda za michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA na kalenda TFF.
Matokeo mengine katika kundi B yanaonyesha kuwa Mbeya ilifungwa na Mwanza magoli 2-5, Pwali iliifunga Iringa 4-0, Lindi ikaifunga Mtwara 2-1, Simiyu imeifunga Iringa 2-0 na Mbeya imeifunga Mtwara 1-0.
Katika matokeo ya kundi A Tanga iliichapa Singida 4-0, Dodoma iliifunga Mara 2-1, Dar es salaam na Kilimanjaro zilitoka sare 1-1, Singida na Kilimanjaro wametoka suluhu ya bila kufungana, Mara imefungwa na Dar es salaam 0-1, na Tanga imeifunga Dodoma 2-1.
Katika kundi C linaloundwa na timu za mikoa ya Geita, Kigoma, Manyara, Njombe, Shinyanga, na Ruvuma, matokeo yanaonyesha kuwa Geita iliifunga Kigoma 1-0, Manyara iliifunga Njombe 2-1, wakati ambapo Shinyanga ilifungwa na Ruvuma 0-2, Kigoma iliifunga Ruvuma 1-0, Njombe iliichapa Shinyanga 4-1, Geita iliifunga Manyara 2-0.
Katika michuano hiyo inayoendelea hapa Mtwara katika kundi D Katavi ilifungwa na kagera 1-2, Moro ilifungwa na Tabora 1-2, Rukwa iliifunga Songwe 3-1 Morogoro na Rukwa zilitoka sare1-1, Kagera iliifunga Arusha 3-0 na katavi na Tabora zilitoka ya bila kufungana.
Kwa upande wa soka wasichana Dar es salaam na Lindi zilitoka sare ya goli 1-1, Kilimanjaro iliichapa Ruvuma 4.30, Ruvuma na katavi zilitoka suluhu ya bila kufungana na Dar es salaam iliichapa katavi.
Pia Tabora iliifunga Simiyu 1-0, Manyara iliifunga arusha 4-0, Aruaha ilitoka suluhu na singida 0-0, Tabora ilifungwa na Manyara kwa 0-1.
Katika kundi A wasichana, Dar es salaam ilitoka sare ya 1-1 na Lindi, Katavi ilifungwa na kagera 1-2, Kilimanjaro ilishinda Ruvuma 4-0, Ruvuma na Katavi zilitoka sare ya bila kufungana na Dar es salaam iliwafunga Kilimanjaro 3-1.
Katika kundi B Tabora iliifunga Simiyu 1-0, Manyara iliifunga Arusha 4-0, Arusha na Singida zilitoka suluhu Na Tabora ilifungwa na Manyara 0-1.
Matokeo ya kundi C wasichana Mwanza iliifunga Iringa 3-0, Kagera na Geita zilitoka sare 2-2, Mwanza na Kagera 1-1 na Geita iliichapa Mbeya 1-0 na kundi D shinyanga ilifungwa na Morogoro 1-3 na Morogoro iliifunga Rukwa 2-1
Kundi maalum Kigoma ilifungwa na Njombe 1-3, Shinyanga ilifungwa na Kilimanjaro 1-3, shinyanga ilifungwa na kilimanjaro 2-3, Kilimanjaro iliifunga Rukwa 10-0 na kigoma iliifunga shinyanga 1-0.
Katika kundi B maalum Tabora iliifunga Kagera 2-1, Manyara iliifunga katavi 7-0, Katavi ilifungwa na Singida 0-5 na tabora na manyara zilitoka suluhu
Katika kundi C maalum matokeo yanaonyesha Mwanza walifungwa na Dodoma 0-1, Tanga imeifunga geita 4-1, Mwanza na Tanga zilitoka sare na Geita ilifungwa na Mtwara 0-4.
Matokeo ya kundi D yanaonyesha Iringa iliifunga mara 1-0, Dar es salaam ilifungwa Ruvuma na irina ilichabangwa bna DSM 0-8
0 Comments