Windows

Msuva: Tutakufa na Senegal Leo

Simon Msuva

MSHAMBULIAJI nguli wa Taifa Stars, Simon Msuva amewataka Watanzania wote kutokuwa na wasiwasi na mchezo wa leo wa Afcon dhidi ya Senegal kwani wamejipanga vilivyo.

 

Taifa Stars leo saa 2 usiku itashuka uwanjani kupambana na Senegal katika mchezo wake wa kwanza katika fainali hizo utakaochezwa kwenye Uwanja wa 30 June huko nchini Misri.

Msuva ambaye ni winga za zamani wa Yanga ameliambia Spoti Xtra kuwa; “Jambo kubwa kwa Watanzania wenzangu ni dua zao ili tuweze kuwa na nguvu za tupambana kwa dakika zote 90 na kupata ushindi.”

“Kuhusiana na maandalizi, tumejiandaa vizuri na kila mmoja wetu ana morali ya juu kwa ajili ya mchezo huo ni matumaini yangu kuwa tutafanya vizuri,” alisema Msuva ambaye anacheza soka la kulipwa nchni Morocco.

SAMATTA, KOCHA Amunike Wafunguka Mchezo VS Senegal

The post Msuva: Tutakufa na Senegal Leo appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments