Windows

Mnaomsubilia Wolper Mmefeli

Jacqueline Wolper Massawe.

MKali wa sinema kunako Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe ametoa povu kwa wale wanaosubiria kwenye peji yake ya instagram kuona kama atamposti mpenzi wake wa sasa na kusema hao wamefeli.

 

Wolper aliliambia Gazeti la ijumaa kuwa, mambo hayo alikuwa akiyafanya zamani kabla ya ufahamu kukomaa, lakini kwa sasa hawezi kufanya hivyo kwani amejitambua.

 

“Nawajua watu ambao kila kukicha wanakodoa macho kuona kama nimemposti nani kwenye peji yangu ya Insta na wanataka kujua nitamtambulisha lini ila wamechelewa kwani hayo mambo yameshapitwa na wakati kwangu,” alisema Wolper ambaye mara ya mwisho alikuwa akitoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’.

The post Mnaomsubilia Wolper Mmefeli appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments