KUTOKaNa na usajili wa kutisha ambao unafanywa na Yanga hadi sasa kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao, mshambuliaji Mkenya Duke Abuya ameweka wazi kwamba naye karibuni anaweza kuwa miongoni mwao.
Mkenya huyo amekoshwa na aina ya usajili ambao unafanywa na viongozi wa Yanga ambapo hadi sasa wameshawapa mikataba wachezaji sita.
Wachezaji hao ambao wamesajiliwa ni Lamine Moro, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Abdulaziz Makame, Ally Mtoni na kipa Metacha Mnata. Mshambuliaji huyo ambaye anaichezea Kariobang Sharks amefunguka kwamba anaweza kutua Yanga kutokana na mazungumzo kati yake na viongozi wa Yanga kuendelea ambapo kama wakifikia muafaka anaweza kusaini.
“Bado maongezi kati yangu na Yanga yanaendelea maana ndiyo tumemaliza mchezo wa ligi kuu hapa nchini (walimaliza Jumapili iliyopita).
“Kwa hiyo yote yanawezekana, mimi kutua katika klabu hiyo kwa msimu ujao,” alisema mshambuliaji huyo. Kariobang walimaliza ligi ya Kenya Jumapili iliyopitan kwa kucheza na Bandari FC ambapo walipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.
The post Mkenya Atangaza Kutua Yanga appeared first on Global Publishers.
0 Comments