Windows

Mexico: Polisi wanene kufukuzwa kazi


Maafisa wa polisi wanaotaka kujiunga na kikosi kipya cha ulinzi wa taifa nchini Mexico wamepewa hadi miezi sita kupunguza uzani la sivyo wafutwe kazi.

Maafisa hao wamepewa agizo hilo wanapoendelea na shughuli ya kukabiliana na wahamiaji haramu.

Maafisa 625 tayari wamefeli vigezo vya kiafya vya kujiunga na kikosi hicho kitakachohudumu katika mpaka wa Kaskazini na Kusini mwa nchi hiyo kwa miezi sita au zaidi, lilisema gazeti la El Financiero katika ripoti yake.

Maafisa ambao hawatafikia vigezo hivyo watalazimika kubaki katika vitengo vingine vya ulinzi wa taifa lakini pia wanakabiliwa na tishio la kufutwa kazi kwasababu kuna mpango wa kuunganisha idara ya polisi na vitengo vingine vya ulinzi kufikia mwisho wa mwezi Juni.

Taarifa hiyo ilifichuka baada ya kanda ya rekodi yenye sauti ya kamanda wa polisi Raúl Ávila Ibarra, iliyovujishwa kupatikana na gazeti la El Universal.

Katika kanda hiyo afisa huyo wa ngazi ya juu anasikika akijaribu kuwashawishi maafisa wadogo kujiunga na na kitengo kipya cha huduma ya uhamiaji huku akiwaelezea kuwa kitengo hicho kipya kinalipa vizuri kuliko chao polisi ".

"Wengine wetu tulio na uzani mkubwa tuna hadi miezi sita kubuni mbinu ya kufukia masharti tuliyopewa," Bw. Ávila Ibarra alisikika akisema.


Post a Comment

0 Comments