Windows

Kauli ya Jaguar yatua ndani ya Bunge la EALA


Adan Mohamed ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kanda wa Kenya ameliambia Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kuwa nchi yake imejizatiti kikamilifu mwanachama mwaminifu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) licha ya matamshi yaliyotolewa na mbunge wa Starehe, Charles Njagua  maarufu ‘Jaguar’.

Alitoa msimamo huo wa Serikali ya Kenya wakati wa kikao cha Bunge kuwa matamshi yaliyotolewa na mbunge huyo yamekera viongozi katika nchi yake pamoja na viongozi wengine kwenye kanda nzima ya EAC.

Waziri Mohamed alinukuu maneno ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliyoyatoa bungeni Juni 25, 2019 kuwa nchi zote zimedhamiria kuwa katika jumuiya hiyo ya kikanda na wanachama wake wasikubali kauli zenye kupanda mbegu za chuki kwa sababu wao ndugu katika jumuiya hiyo.

“Napenda kurejea msimamo wa Serikali ya Kenya kuwa msimamo wetu hautikisiki kuhusu mtangamano wa Jumuiya yetu, mkataba ulioanzisha EAC na itifaki zake ambayo tumeiridhia bado itaendelea kuiheshimu ikianzia na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta,” alisema

“Mheshimiwa Spika na Bunge zima kama mnavyo fahamu, Rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara amekua akizungumza hadharani akiwakaribisha wananchi wa Afrika Mashariki kwenda kuwekeza, kutembelea vivutio vyetu na hata kuoa na kuolewa na kuweka makazi yao huko ili mradi wanafanya hivyo kwa kuzingatia sheria,” alisema Mohamed.

Post a Comment

0 Comments