MABINTI watatu wa mkongwe katika Muziki wa Hip Hop, P Diddy, D’Lila, Jessie na Chance wametokelezea na vitu vyenye thamani ya dola 50,000 (zaidi ya shilingi milioni 114 za Kibongo) kwa usiku mmoja.
Mabinti hao walitokelezea katika uzinduzi wa filamu mpya ya The Secret Life Of Pets 2 ndani ya Ukumbi wa Regency Village Theatre uliopo Westwood, California.
Katika mabinti hao, kuna pacha wawili, D’Lila na Jessie ambao walitinga vibegi vya mgongoni aina ya Hermes vilivyotengenezwa kwa kutumia ngozi ya chatu vyenye thamani ya dola 22,000 kila kimoja (zaidi ya shilingi milioni 100 kwa viwili) na dada yao, Chance alitinga na kipochi cha njano aina ya Christian Louboutin yenye thamani ya dola 5,000 (zaidi ya shilingi milioni 11).
Pacha D’Lila na Jessie’s mom walizaliwa na marehemu, Kim Porter lakini Chance alizaliwa na Sarah. Kwa sasa wote watatu wanalelewa na Sarah.
CALIFORNIA, MAREKANI
The post Mabinti wa P Diddy watokelezea na Mil.114 appeared first on Global Publishers.
0 Comments