Kada ya Mawasiliano Serikalini imetajwa kuwa chachu ya kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano .
Akizungumza wakati wa ziara yakuwatembelea na kuona utendaji wa maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wa Mashirika na Taasisi zilizopo Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano (TAGCO) Bi Sarah Kibonde amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa maafisa hao kutumia mbinu za kisasa kutangaza mafanikio ya Serikali.
“Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanatangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano hasa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi hivyo tunawakumbusha wajibu huu wa msingi ” Alisisitiza Bi Kibonde.
Akifafanua Bi Kibonde amesema kuwa kwa sasa Serikali imewekeza katika miradi mingi ya maendeleo katika sekta zote zinazolenga kuleta ustawi wa wananchi na jukumu la kuitangza ni la kada hiyo.
Kwa upande wake muwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO katika ziara hiyo Bw. Casmir Ndambalilo amesema kuwa Idara hiyo imejipanga na iko tayari kuendelea kuwajengea uwezo maafisa habari wote pale wanapohitaji ili kuwaongezea ujuzi zaidi.
0 Comments