LIVERPOOL jana ilitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya sita baada ya kuiliza Tottenham Spur mabao 2-0 kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopigwa kwenye Uwanja wa |Wanda Metropolitano jijini Madrid nchini Hispania.
Miamba hiyo sasa imeongeza taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye kabati lao baada ya kuwahi kunyakua taji hilo katika miaka ya 1977, 1978, 1981, 1984 na 2005.
Liverpool angalau ilifuta machozi ya kupoteza fainali ya msimu uliopita wa 2017/18 wakati walipofungwa mabao 3-1 na Real Madrid mjini Kiev nchini Ukraine. Mabao ya Liverpool katika fainali hiyo yalipachikwa na Mohamed Salah na Divock Origi.
Liverpool ilipata bao la kwanza mapema dakika ya pili likifungwa kwa penalti na Salah. Penalti hiyo ilitokana na kiungo Moussa Sissoko kuunawa mpira kwenye eneo la hatari baada ya kugongeshewa mpira mkononi na fowadi wa Liverpool, Sadio Mane.
Hata hivyo, penalti hiyo ilizua ubishi kwa Sissoko mwenyewe kudai kuwa mpira ulikuwa umemgonga kifuani ingawa picha za televisheni zilionyesha mpira ulimgonga mkononi kutokana na ukweli kuwa mwenyewe alikuwa amenyoosha mkono juu.
Bao hilo limeingia katika orodha ya mabao ya mapema zaidi kufungwa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ingawa halikufi kia lile la Paolo Maldini, ambaye alifunga chini ya dakika ya kwanza wakati akichezea AC Milan ilipokabiliana na Liverpool kwenye fainali ya mwaka 2005.
Baada ya kufungwa bao lile, Tottenham walijitahidi kutafuta bao lakini walikuwa wanakwama kuupenya ukuta mgumu wa Liverpool, ambayo wachezaji wake walikuwa wanakaba zaidi. Tottenham wazuri katika kumiliki mpira lakini Liverpool walikuwa walikuwa wanasubiri kufanya mashambulizi ya kushitukiza `counter attack’.
Straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane alifi chwa muda mwingi wa mchezo huo, ambapo mathalani katika kipindi cha kwanza aligusa mpira mara 11 tu. Mnamo dakika ya 38, Liverpool ilipiga `counter attack’, ambapo beki Andrew Robertson alipanda mbele na kupiga shuti kali lililopanguliwa na kipa wa Tottenham Hotspur, Hugo Lloris.
Tottenham ilipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha dakika ya 83 baada ya kupata faulo karibu na eneo la Liverpool lakini kipa Alisson alipangua mpira uliopigwa na Christian Eriksen na kuzaa kona.
Origi aliimaliza Tottenham kwa kuendeleza kawaida yake ya kupachika mabao katika dakika za mwisho baada ya kupachika bao la pili la Liverpool katika dakika ya 88, ambapo alifunga kwa shuti kali la chini baada ya kupata mpira kwenye eneo la hatari la Tottenham. Hii ni mara ya nne kwa Origi kupachika bao katika dakika ya mwisho msimu huu kama alivyofanya kwenye mechi za dhidi ya Everton, Newcastle na Barcelon
The post LIVERPOOL NDIO MABINGWA ULAYA, YAIPIGA TOTTENHAM 2-0 (Picha +Video) appeared first on Global Publishers.
0 Comments