Windows

Kambi ya Yanga Bab Kubwa

WAKATI Yanga wakiwa wanakamilisha zoezi la usajili ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao imebainika kwamba viongozi wa timu hiyo chini ya mwenyekiti wake, Mshindo Msolla wanaandaa kambi babkubwa itakayokuwa ugenini kwa ajili ya kikosi hicho.

 

Yanga wana mipango ya kuanza kambi mapema kama agizo la kocha wao Mwinyi Zahera ambaye anataka timu hiyo iunge vizuri kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Bara msimu ujao.

 

Kambi hiyo ya timu ya Yanga itaanza Julai 7, ambapo itakuwa nje ya Dar, ambapo Zahera anataka sehemu tulivu kwa ajili ya ‘kuyafua’ majembe yake mapya.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela ameliambia Spoti Xtra kuwa, wapo kwenye mipango kabambe ya kuhakikisha wanaifanya kambi hiyo kuwa ya kipekee huku wakitumia kiasi cha milioni 930 ambacho walikipata hivi karibuni kutokana na michango ya timu hiyo.

 

“Sasa tunamaliza masuala ya usajili ambapo tupo kwenye hatua za mwisho kabisa kabla hatujakamilisha suala hilo na tutahamia kwenye kambi. “Kambi yetu itakuwa Julai 7, lakini tunaifikiria kuwa kambi ya kitofauti ambapo tutaenda nje ya Dar lakini tutatumia baadhi ya fedha kwenye zile milioni 930 ambazo tumezipata hivi karibuni kulikamilisha suala hilo.

 

“Tunataka kambi ya mapema ili kuwafanya wachezaji wakae sehemu moja na waunde timu kwa ajili ya ligi na ya kimataifa ambapo ni muhimu zaidi,” alisema Mwakalebela ambaye anaishi Sinza kwa Wajanja Jijini Dar es Salaam

SAID ALLY, Dar

The post Kambi ya Yanga Bab Kubwa appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments