Windows

Kalengo dogo mwenye kipaji aliyetua Yanga



Yanga imekamilisha usajili wa mshambuliaji kinda Maybin Kalengo kutoka ZESCO United ambaye juzi alisaini mkataba wa miaka miwili kisha kurejea kwao Zambia kumaliza majukumu na kikosi cha ZESCO

Inaelezwa ujio wa Kalengo umefanikishwa na Noel Mwandili kocha msaidizi wa Yanga baada ya kupata ridhaa ya George Lwandamina ambaye kwa sasa ndiye kocha Mkuu wa ZESCO

Kalengo anafahamika sana Zambia kwani alianza kun'gara tangu alipokuwa na umri wa miaka 16 akicheza timu ya Taifa ya vijana

Aidha kinda huyo amekulia kwenye familia ya soka kwani mjomba wake Winston Kalengo aliwahi kucheza timu ya Taifa ya Zambia na ameitumikia ZESCO United kwa muda mrefu

Kalengo ni mshambuliaji mwenye kipaji, ana nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kufunga mabaocut

Kipaji cha Kalengo kilivumbuliwa mwaka 2014 na Airtel Rising Stars ambapo katika mashindano yaliyoandaliwa na Airtel, aliibuka kuwa mfungaji bora na mchezaji bora

Akiwa kikosi cha ZESCO, Kalengo amepata uzoefu wa mechi za Kimataifa kwani alishiriki mpaka mechi za ligi ya mabingwa

Ni mshambuliaji mwenye malengo ya kufika mbali, nafasi hii aliyoipata katika klabu ya Yanga inaweza kumsaidia kufikia ndoto zake

Wapo wanaojiuliza kwa nini Yanga imemsajili kinda huyo huku wakiwa hawaamini kama ataweza kumudu mikiki ya ligi ya Tanzania

Lakini wasichofahamu ni kuwa Kalengo alianza kucheza ligi kuu Zambia akiwa na umri wa miaka 17 na katika kikosi cha ZESCO ameaminiwa na Lwandamina ambaye amemtumia katika michezo mingi

Lakini pia ni utamaduni wa Yanga kusajili na kuwapa nafasi wachezaji chipukizi.

Mfano mzuri ni Ramadhani Kabwili, Yohana Mkomola, Paulo Godfrey 'Boxer', Gustapha Saimon, Abdallah Shaibu na Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye msimu uliomalizika, alikuwa tegemeo katika kikosi cha Yanga licha ya kuwa na umri wa miaka 20 tu

Post a Comment

0 Comments