Windows

Gigy Money acharuka kuhusu mwanaye

Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’.

 

BAADA ya kuvuja video ikimuonesha akicheza na mwanaye, Mayra huku mashabiki wakimjia juu kuwa anamharibu, msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amecharuka kwa kusema kuwa atabaki kuwa mwanaye hata waseme vipi.

 

Juzikati kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gigy aliposti kipande cha video akiwa na mwanaye wakicheza ambapo kwa mtazamo wa mashabiki walisema kuwa alikuwa akimharibu kutokana na staili aliokuwa akicheza naye.

Akizungumza na Shusha Pumzi, Gigy alicharuka kwa kusema; “Watu wengine sijui wakoje, mimi nashaangaa watu wamenitolea povu weee kwani hakuna mzazi ambaye anacheza na mwanaye? Mimi niliamua tu kucheza na mwanangu kama wengine wanavyofanya ila ndiyo kila mtu ana mtazamo wake sidhani kama kucheza kuna tatizo tena wanitue.

EXCLUSIVE: ROSE NDAUKA Afunguka USIYOYAJUA “MIMI SIRIDHIKI”

The post Gigy Money acharuka kuhusu mwanaye appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments