TIMU ya Esperance ya Tunisia imetangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Mabingwa Afrika usiku wa kuamkia leo baada ya mchezo wa pili wa marudiano dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco kuvunjika dakika ya 59 kipindi cha pili baada ya Wydad kusawazisha na bao hilo kukataliwa kwa kuwa lilikuwa ‘offside’.
Wachezaji wa Wydad Casablanca ndiyo wamesababisha mchezo huo kushindwa kumalizika na matokeo yake Esperance kutawazwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo.
Kabla ya fainali ya pili ya marudiano, matokeo yalikuwa 1-1.
Katika fainali hiyo ya marudiano timu ya Esperance ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Youcef Belaili dakika ya 41 kipindi cha kwanza na dakika ya 59 kipindi cha pili Wydad Casablanca walisawazisha na bao lao kukataliwa na kuamini kuwa wanaonewa na kugomea kuendelea na mchezo huo.
Hata hivyo, mechi hiyo imeonekana kuwashinda marefa wengi baada ya refa wa kwanza raia wa Misri aliyechezesha mchezo wa kwanza kusimamishwa kwa miezi sita kwa madai kuwa alichezesha akiwa chini ya kiwango, hivyo ilivyotokea leo ikawa rahisi kwa Wydad kuhisi wanaonewa hususani pale mwamuzi alipokataa kwenda hata kuangalia VAR ili aweze kutengua au kuendelea na uamuzi wake.
The post Esperance Wapewa Ubingwa Baada ya Wydad Kugomea Mechi appeared first on Global Publishers.
0 Comments