NGULI wa Muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes ‘Mr Misifa’, jana Alhamisi alitembelea Ofisi za Global Group na kushangazwa na maendeleo ya kampuni hiyo huku akitoa tano kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Eric Shigongo.
Dully Sykes licha ya kutembelea ofisi hizo pia alikuwa akitambulisha wimbo wake wa Nikomeshe aliofanya na msanii Harmonize kutoka Lebo ya WCB.
Staa huyo asiyechuja, alizungumza mbele ya kipaza sauti cha Kituo cha +225 Global Radio ambapo lengo likiwa ni kuutambulisha wimbo huo lakini mapokezi aliyoyapata na maendeleo aliyoyakuta alijikuta akitoa tano kwa Shigongo.
Akiuzungumzia wimbo wake wa Nikomeshe, Dully alisema: “Huu wimbo nimefanya na Harmonize na watu wengi wanashangaa kwa nini nafanya naye kazi nyingi, labda niwaambie kuwa mimi Issa Liponda Dar es Salaam na Harmonize ni washirika wa kibiashara (business partners), kwa hiyo yeye anaweka hela na mimi naweka.”
Kuhusu Shigongo, Dully alisema: “Unajua lazima ufanye kazi kwa ushirikiano ili ufanikiwe, labda nikuambie kuwa huyu Shigongo wakati anaanzisha hii kampuni mwaka 1999 mimi nilikuwepo na sisi ni watu wa mwanzo kufanya naye kazi.
“Alikuwa na ofisi ndogo tu kama hii studio na wakati huo kupata kompyuta ilikuwa ni shida, ulikuwa ukiingia katika ofisi yake unakuta kompyuta zipo mbili tu na meza moja basi, lakini nimeshangaa leo kuona ana ofisi kubwa yenye watu wengi tofauti na nilivyokuwa nafikiria.
“Maana yake alifanya kazi na watu kwa ushirikiano na hatimaye akayafikia haya mafanikio, ndivyo ilivyo kwangu mimi na Harmonize na kazi zipo nyingi siyo hiyo peke yake.”
Kusikiliza matangazo ya +255 Global Radio ‘live’ fungua mtandao katika anwani hii: 255 Global Radio App hakikisha uwe na bando japo kidogo tu. Mahojiano hayo kwa urefu yanapatikana kwenye YouTube katika Chaneli ya Global TV Online.
The post DULLY SYKES AFICHUA SIRI YA KUFANYA KAZI NYINGI NA HARMONIZE appeared first on Global Publishers.
0 Comments