Mkongoman, huyo amesisitiza hatanyamaza kusema ukweli kwa kitu anachokiona akiendi sawa na kusema idadi kubwa ya viporo alivyokuwa nao Simba ni mambo yaliyopunguza ushindani na kutengeneza bingwa wa msimu huu.
Alisema hawezi kunyamaza wakati ukweli ndivyo ulivyo na kudai vi vyema tu TFF ikawapa tu Simba taji lao kwao Yanga haina nafasi kwa vile wenzao wana mechi nyingi mkononi.
Kocha huyo, alisema ni ngumu kuwa na ushindi wa kutosha kwenye Ligi kama kuna kuwa na wimbi kubwa la viporo ambavyo kwa namna moja ama nyingine vinatafsiriwa vib“Kuna kipindi Yanga ilicheza mechi 15 huku timu nyingine zikicheza mechi saba, sio sawa kabisa, mbona kuna Ligi za mataifa mengine ambayo yapo hapa hapa Afrika lakini hakuna matatizo ya ratiba na timu zao zimekuwa zikishiriki kwenye mashindano ya kimataifa,” alisema kocha huyo.
“Nimeipenda Ligi ya Afrika Kusini, siku ya mwisho ndio iliyotumika kutangazwa bingwa wa msimu huu, nilipenda na hapa hata kama atatangazwa mapema isiwe kwa kisingizio cha ratiba iwe kwa kuzidiwa uwezo.”
Zahera na wanamichezo wengine nane walishtakiwa na Bodi ya Ligi kwa makosa ya utovu wa nidhamu ambapo Jumapili iliyopita kamati ilikutana kuwasikiliza na hukumu zao hazijatoka.
0 Comments