KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesisitiza kuwa straika wa timu hiyo, Heritier Makambo hajauzwa na bado ni mali ya klabu hiyo. Zahera alisema jana kuwa hakuna dili lolote lililofanyika baina ya straika huyo na timu ya Horoya A.C ya Guinea na hata akiondoka basi fedha yote itakwenda kwenye klabu ya Yanga
Hivi karibuni kulizagaa taarifa kuwa Makambo amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuchezea timu hiyo ya Guinea, ambayo ilishiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Kocha huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo alikiri kuwa Makambo alikutana na viongozi wa klabu hiyo lakini sio kwa ajili ya kusaini mkataba.
“Ni kweli tulikutana na uongozi wa Horoya na ilikuwa baada ya kupata usumbufu mkubwa wa kutafutwa lakini hakuna dili lolote lililofanyika na ikitokea basi fedha yote itakuwa mali ya yanga” alisisitiza Zahera
The post ZAHERA: MAKAMBO NI MALI YA YANGA appeared first on Global Publishers.
0 Comments