


Jana ligi kuu soka ya Tanzania bara ilimalizika kwa Simba kutwaa ubingwa wao na Yanga kushika nafasi ya pili huku Azam Fc wakishika nafasi ya tatu.
Baada ya mchezo kati ya Yanga na Azam fc kumalizika kocha mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi alipata nafasi ya kuzungumza kuhusu ligi na usajili kiasi ndani ya kikosi cha Yanga.
Zahera Mwinyi aliulizwa swali kuhusu mchezaji wa Simba Said Ndemla kama atatua ndani ya Yanga na kocha huyu alisema hana jina la Ndemla katika list yake.
“Said Ndemla hayupo kwenye makaratasi yangu sina habari zake.”



0 Comments