Windows

Yanga yatoa shukrani kwa wadau wake


Hizi ni shukrani kutoka kwa Mabingwa wa kihistoria;

Uongozi wa Yanga, unatoa shukrani na pongezi za kipekee sana kwa Mwalimu Mwinyi Zahera na benchi lote la ufundi pamoja na wachezaji wetu waliopambania timu yetu katika jua na mvua, katika majani, vumbi na tope, nyumbani na ugegenini.

Tunatambua ukali wa mapambano yao na changamoto za hapa na pale, lakini tumeweza kumaliza msimu na na alama 86, tukiachwa alama chache na mshindi wa kwanza.

Asante na hongereni sana majemedari.

Lakini Yanga si kitu bila wanachama wake, washabiki na wadau wote wanaojitolea kuipa nguvu timu yetu.

Sisi uongozi, tunathamini na kushukuru sana nguvu zenu kwenye majukwaa ya viwanja, majumbani na sehemu zote mnapotutazama na kutusikiliza tukicheza, na kwa maoni yenu mnayotoa kwa njia mbalimbali bila kusahau michango ya fedha.

Hakika hii ni timu ya Wananchi, tutazidi kusonga mbele

Na sasa, uongozi unawaahidi Yanga KUBWA KULIKO: tutaanza msimu mpya na Yanga Mpya

Hakika, katika mioyo ya Wanajangwani, washindi wa kweli ni utatu imara wa Yanga yaani wa kwanza KOCHA NA BENCHI LA UFUNDI, pili WACHEZAJI na tatu ni WASHABIKI NA WANACHAMA WA YANGA.

Hongera kwetu sote:

Post a Comment

0 Comments