YANGA Leo imeyaaga mashindano rasmi ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kukubali kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli mchezo uliochezwa uwanja wa Samora.
Lipuli iliyo chini ya Kocha Sele Matola ilitumia dakika 45 kuumaliza mchezo kwani walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili hali iliyofanya kuwapa nguvu ya kurejea kipindi cha pili kulinda mabao yao hayo.
Dakika ya 29 Paul Nonga aliandika bao baada ya mlinda mlango wa Yanga Klaus Kindoki kutema mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Lipuli, Miraji Athuman ukazama kabla ya dakika ya 39 mabeki tena kujichanganya na kumuachia Miraji Athuman kuandika bao la pili kwa Lipuli.
Jitihada za Lipuli kusawazisha mabao hayo kipindi cha pili ziligonga mwamba licha ya kuonesha nia ya kutafuta mabao ukuta wa Lipuli uliokuwa chini ya Ally Mtani ulizuia mashambulizi yote ya Yanga.
Makosa ya safu ya ulinzi wa Yanga iliyokuwa chini ya Abdallah Shaibu 'Ninja' yameigharimu Yanga na kupoteza mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kurejea Dar kujiandaa na michezo yao ya Ligi ili kuendelea kwenye mbio za ubingwa ambao ushindani wake umezidi kuwa mkubwa kwa timu tatu za juu ambazo ni pamoja na Simba na Azam FC.
Fainali itawakutanisha Azam FC na Lipuli itakayochezwa uwanja wa Ilulu, Lindi na mshindi wa michuano hii ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

0 Comments