Yanga imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Lipuli Fc kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Samora mkoani Iringa
Makosa yaliyofanyika kwenye kipindi cha kwanza ndio yaliyoigharimu Yanga kwa kuruhusu mabao mawili yaliyofungwa na Paul Nonga na Saliboko
Licha ya kutafuta mabao ya kusawazisha kwenye kipindi cha pili, Lipuli Fc ilikuwa imara katika kujilinda
Matokeo hayo yameondosha matumaini ya Yanga kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao kwani nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ni kama haipo, watani zao Simba wanaelekea kutwaa ubingwa huo
Lipuli Fc sasa itachuana na Azam kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa Juni 02 uwanja wa Ilulu mkoani Lindi

0 Comments