Taarifa kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo, Patrick Gakumba, amesema tayari walishaongea na Yanga na aliwapa masharti ya kuhakikisha analipwa milioni 18 kwa mwezi.
Baada ya kutolewa kwa masharti hayo, mpaka sasa Yanga wameonekana kuwa kimya lakini vilevile zimekuja taarifa za Vita kutaka namba ya mchezaji huyo.
Vita ambao ni vinara wa Ligi Kuu Congo hivi sasa wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Tuyisenge kutokana na ukubwa wa klabu yenyewe pamoja na kuwa na mpunga mwingi tofauti na Yanga,
Hii si mara ya kwanza kwa taarifa za mchezaji huyu kutajwa kutua Yanga lakini vilevile miezi kadhaa iliyopitwa Simba SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara nao walitajwa kutaka saini ya mchezaji huyo ila baadaye uongozi ukakanusha taarifa hizo.
0 Comments