Windows

Yanga kukamilisha ukarabati uwanja wa Kaunda


Uongozi wa klabu ya Yanga umeandaa mpango wa muda mfupi ambao utawezesha ukarabati wa uwanja wa Kaunda ili uweze kutumika kwa ajili ya mazoezi
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema baada ya msimu kumalizika wataanza ukarabati wa sehemu ya kuchezea 'pitch' ya uwanja wa Kaunda ili uweze kutumika msimu ujao
"Kwa sasa tutakarabati sehemu ya kuchezea, ni zoezi ambalo litachukua takribani miezi mitatu," amesema Mwakalebela
"Lengo letu ni kuhakikisha msimu ujao tunakuwa na uwanja wetu wa mazoezi ili kupunguza gharama"
"Gharama tunazotumia kukodi viwanja ni kubwa, pesa hiyo inaweza kutusaidia katika masuala mengine yakiwemo ya usajili"
Kuhusu adha ya mafuriko Jangwani, Mwakalebela amesema kifusi kilichowekwa mwanzo kimepunguza adha hiyo na wanakusudia kuongeza kifusi kingine kabla ya kuanza mchakato wa kupanda nyasi sehemu ya kuchezea

Post a Comment

0 Comments