Usiku wa kuamkia leo Wydad Casablanca iligoma kuendelea na mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Esperance baada ya kukataliwa bao la kusawazisha kwenye dakika ya 59
Mpaka wakati wa mapumziko timu hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 lakini bao hilo lililokataliwa lingefanya matokeo yawe 1-1 sawa na mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Morocco
Baada ya bao lao kukataliwa na mshika kibendera kwa sababu ya Offsise, Wydad walimtaka mwamuzi akatizame picha za marudio za VAR ili ajiridhishe
Hata hivyo ikabainika kuwa mfumo wa VAR haukuwa ukifanya kazi
Majadiliano yalifanyika kwa karibu saa zima bila ya mafanikio, Wydad wakigoma kurejea uwanjani
Mwamuzi alimaliza mchezo na Esperance kutetea taji la ligi ya mabingwa barani Afrika kwa msimu wa pili mfululizo
Picha za marudio za televisheni zinaonyesha Kharti, mfungaji wa bao la Wydad hakuwa ameotea hivyo bao hilo lilikuwa sahihi
Lakini kituko kikubwa ni mfumo wa VAR kutofanya kazi licha ya kuwepo uwanjani hapo
Mfumo huo ulitumika kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Morocco ambao ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1
0 Comments