

Aliyewahi kuwa mkufunzi wa Arsenal, Arsene Wenger amesema yuko tayari kurejea kwenye uongozi wa soka lakini sio kufundisha
Wenger alimaliza miaka yake 22 ya kuwa kocha wa Arsenal mwishoni mwa msimu wa 2017-18.
Awali alitarajiwa kurejea tena katika majukumu hayo mwanzoni mwa mwaka 2019
Lakini Wenger mwenye umri wa miaka 69, aliiambia BBC kuwa kwa sasa anafurahia maisha nje ya soka ingawa mwanzo alidhani angerejea katika majukumu ya ukocha muda mfupi baada ya kuondoka Arsenal
"Nilidhani nitarudi katika ukocha haraka sana lakini nimefurahia maisha nje ya soka"
"Sasa niko njia panda," amesema Wenger
"Sina hakika kama nitarejea tena majukumu ya ukocha"
"Mwaka huu nimefanya kazi nyingi za kujitolea, nimefurahia maisha. Nimependa kuwa nje ya vyombo vya habari na kutokuwa na msongo wa mawazo"
"Nitarejea uwanjani hivi karibuni lakini siwezi kukwambia ni katika nafasi gani"



0 Comments