Windows

Wawa arejea kikosini Simba


Beki kisiki wa Simba Paschal Serge Wawa amerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa mwezi mmoja akiuguza majeraha ya nyama za paja
Wawa tayari ameanza kujifua na kikosi cha Simba kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Azam Fc utakaopigwa kesho
Hata hivyo Wawa hatarajiwi kushuka dimbani kesho kwa kuwa amepewa program maalum ya mazoezi ya pekee yake ambao ametakiwa kuyafanya kwa siku nne
"Nimeanza mazoezi. Kwa sasa nafanya mazoezi ya peke yangu kwa siku nne kabla ya kujiunga na wenzangu," amesema
Wawa aliumia kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe uliopigwa April 06 katika uwanja wa Taifa
Beki huyo mkongwe huenda akarejea kikosini kwenye mchezo dhidi ya Ndanda Fc na bila shaka atakuwepo Simba itakapochuana na Sevilla kwenye mchezo wa kirafiki, May 23

Post a Comment

0 Comments