Windows

Usajili Yanga wamtisha Ngasa



Winga wa Yanga Mrisho Ngasa amesema amekuwa akifuatilia, na ameridhishwa na usajili unaoendelea kufanywa na timu hiyo

Ngasa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri kwenye kikosi cha Yanga msimu uliomalizika, amesema timu hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao

"Nimefurahishwa na usajili unaoendelea, ili mchezaji ufanye vizuri lazima nyuma yako wawepo wachezaji wengine bora, nina imani na usajili huu kuwa ni wachezaji wazuri,"amesema

"Nimetulia nafuatilia usajili, tutatisha msimu ujao, niwaambie wapenzi na mashabiki wa Yanga watulie tutapata timu nzuri baada ya kupata uongozi mpya"

Licha ya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaomaliza mikataba, Ngasa anatarajiwa kuongeza mkataba kuendelea kukipiga na mabingwa hao wa kihistoria

Hata hivyo msimu ujao atakumbana na changamoto ya ushindani wa namba baada ya Yanga kuwasajili mawinga/viungo vijana wenye kasi Patrick Sibomana na Issa Birigimana

Sibomana amesajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Mukura Victory ya Rwanda wakati Birigimana ametokea APR

Wawili hao waliwahi kucheza pamoja APR kabla ya Sibomana kutimkia Ulaya na baadae kurejea Rwanda na kujiunga na Mukura Victory

Post a Comment

0 Comments