Windows

Usajili : Bocco akata mzizi wa Fitna kutua kati ya Simba au Azam



Nyota kadhaa wa klabu ya Simba mikataba yao inamalizika baada ya msimu huu kumalizika.


Simba inampango ya kuachana na baadhi ya nyota wake huku baadhi ya nyota ambao wamekuwa kwenye viwango bora kabisa wakiwa kwenye mipango ya kuongezewa mikataba mpya.

Moja ya nyota ambaye inaelezwa Simba wapokatika mipango ya kumuongezea mkataba ni nahodha wa timu hiyo John Raphael Bocco ambaye mkataba wake unaisha msimu huu.

John Bocco amekuwa akitajwa kuwaniwa na waajiri wake wa Zamani Azam Fc huku mara kadhaa Simba ikielezwa kushindwa kukubaliana naye baadhi ya vitu anavyotaka ili kuongeza mkataba baada ya huu kumalizika.

Mahitaji ambayo amekuwa akiyataka Bocco kwenye mkataba mpya inaelezwa Azam Fc wao wamekuwa wapo tayari kuyatimiza huku Simba wakionekana kusuasua.

Lakini taarifa za ndani ambazo kwata unit imezipata ni kwamba Simba wameshakubaliana na John Bocco na tayari amekubali kuongeza miaka miwili ya kuendelea kuitumikia Simba.a

Post a Comment

0 Comments