Windows

Unahodha wa Gyan bado waitesa Ghana

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana, Nii Odartey Lamptey amemtolea uvivu kocha wa timu hiyo, James Kwesi Appiah kwa kusema huu haukuwa muda sahihi kwa Asamoah Gyan kuvuliwa unahodha.


Lamptey alisema kufanya maamuzi ya kumvua unahodha Gyan mwezi mmoja kabla ya Afcon kunaweza kuigawa Black Stars wakati wa fainali hizo.


“Hesabu za kumvua unahodha ni mbovu, angalia sasa badala ya fikra na mawazo yao kuelekeza kwenye fainali za Afcon, wanaelekeza kwenye suala la unahodha huu ni upuuzi.


“Angemuacha Gyan aipeleke timu Misri baada ya hapo ndio angeamua kufanya uamuzi huyo au angeyafanya basi hayo maamuzi yake miezi sita iliyopita,” alisema mchezaji huyo wa zamani.


Baada ya kuvuliwa unahodha wa kikosi hicho, Gyan amepewa jukumu la kuwa kiongozi kwa wenzake 'General Captaincy' kutokana na ukongwe alionao kwenye timu hiyo.


Akilizungumzia pia jukumu hilo kwa Gyan, Lamptey alisema anachoweza kumshauri ni kuukata unahodha wa ujumla, “Nadhani anaweza kuwa na wasi wasi wa kuukataa kwa sababu atachukulia tofauti.”

Post a Comment

0 Comments