Windows

Tunakusanya fedha za usajili na mishahara - Mutta


Katibu wa Kamati ya Hamasa Deo Mutta amesema tukio la uchangiaji Yanga litakalofanyika Juni 15 2019 ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, ni tofauti na mchakato wa awali uliofanywa na ambapo kamati hiyo iligawa kadi 1500 kwa makundi mbalimbali

Akihojiwa na kpindi cha Yanga TVjuzi, Mutta alisema fedha zitakazopatikana katika tukio hilo zitajumuishwa na zilizopatikana kupitia michango ya kadi 1500 ambazo ziligawiwa kwenye mikoa 30, Makundi ya Mitandao ya kijamii, Taasisi na watu binafsi

Kila kadi ina thamani ya Tsh Milioni moja

Mutta amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana zitatumika kumaliza changamoto zilizopo, kufanya usajili pamoja na kukidhi gharama za uendeshaji wa klabu kwa angalau miezi sita

"Unaposajili wachezaji, wanahitaji kulipwa mishahara hivyo fedha tunazokusanya zitatumika kusajili na kulipa mishahara ya wachezaji," amesema

"Lakini pia fedha hizi zitamaliza changamoto zilizopo kama madai ya baadhi ya wachezaji na changamoto nyingine"cut

Juni 15 Yanga itafanya tukio kubwa la kihistoria ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo wadau wa timu hiyo watashiriki katika Harambee ya kuichangia Yanga

Harambee hiyo itaanza saa nne asubuhi mpaka saa 12 jioni, lengo likiwa kukusanya angalau Tsh Milioni 500

Post a Comment

0 Comments