

Alichokisema Jonas Tiboroha baada ya kushindwa kwa kura katika kugombea nafasi ya Uenyekiti Yanga
Yanga oyeeeeee!! Daima Mbele Nyuma Mwiko.
Napenda nitoe shukrani zangu kwa kamati ya uchaguzi, pili nawashukuru wapiga kura wote hakika wana Yanga mmeongea kwa sauti kubwa sana.
Hatimaye tumempata mwenyekiti, kama mgombea nampongeza sana mwenyekiti na pia namtakia kila la heri katika shughuli yake inayokuja, sio shughuli ndogo ila nna imani kubwa juu yake anaweza kutupeleka kwenye nchi ya ahadi.
Lakini mimi kama mwana Yanga nilishamtumia ujumbe wa pongezi ndugu mwenyekiti kwa kuwa nilishapata matokeo mapema kidogo!
Nimemwambia kabisa mimi kama mwana Yanga nipo tayari kumsaidia pale anapoona nafaa na kunihitaji.
Mwisho kabisa nawapongeza wale watu 60 walionipigia kura kwa maana kura zao zimewezesha kupatikana mshindi, ni muda sasa kuvunja kambi na utimu kuanzia sasa wote ni timu Msolla, Ahsanteni sana"
Na Jonas Tiboroha.




0 Comments