Windows

TFF kutoa ufafanuzi wa timu zilizoshuka daraja



Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura leo anatarajiwa kutoa ufafanuzi wa timu zilizoshuka daraja baada ya ligi kuu ya Tanzania Bara kumalizika hapo jana



Kumekuwa na sintofahamu juu ya timu ipi inapaswa kuungana na African Lyon kushuka daraja kati ya Stand United na Kagera Sugar

Kulingana na takwimu zilizotolewa na Bodi ya Ligi hapo jana, Stand United na Kagera Sugar zote zina alama 44 huku pia zikiwa na tofauti sawa ya mabao -11

Ilielezwa sheria ya 'head-head' ilitumika kuishusha daraja Kagera Sugar

Post a Comment

0 Comments