


Taarifa ambazo sio rasmi zinaeleza kuwa Nahodha wa Simba SC, John Bocco usiku wa jana alisaini mkataba wa miaka miwili.
Hayo yanajiri ikiwa tayari klabu yake ya zamani Azam FC ilikuwa imeonyesha nia ya kuhitaji kandarasi ya msumbuliaji huyo aliyefunga magoli zaidi ya 100 kwenye Ligi ya Tanzania.
Hapo jana John Bocco aliwezesha timu yake kurejea kwenye usukani wa Ligi kwa kuifungia goli la utangulizi dhidi ya Mtibwa Sugar na kuchagia ushindi wa goli 3-0 walioupata na kuwawezesha kufikisha pointi 85



0 Comments