MIAKA ya 1990 hadi 2000, radio na TV ndiyo vilikuwa vyanzo pekee vya kuniweka karibu zaidi na msisimko halisi wa soka. Miaka hiyo ukisikia majina kama Nteze John ‘Rungu’, Ally Mayay ‘Tembele’, Juma Kaseja basi bila shaka unajua wababe wa nchi wanafanya yao kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar kipindi hicho ukijulikana kama ‘Shamba la Bibi’.
Simba na Enyimba, pia Yanga na Zamalek ndiyo zilikuwa mechi kubwa ambazo ukimsikia Juma Nkamia akitangaza pande za RTD basi ni lazima uongeze umakini usipitwe.
SHAUKU INARUDI TENA
Kwa shabiki ambaye amezoea kwenda uwanjani kuiona Simba au Yanga ikicheza mara kwa mara na timu za Tanzania au kutoka nchi nyingine za Bara la Afrika, huwa nakuwa na shauku ya kawaida tofauti na yule ambaye ni mara yake ya kwanza. Leo hii tunazungumzia timu kama Sevilla kutoka nchini Hispania kuja Tanzania kucheza dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Hii ni mechi kubwa ambayo hata kama umeshaitazama Simba uwanjani mara 1000 basi bila shaka ungetamani kuwepo kuona jinsi wababe hao wa La Liga wakicheza soka kwenye ardhi ya Tanzania.
Sevilla inakuwa ni timu ya pili kubwa kutoka barani Ulaya kutembelea Tanzania na kucheza mchezo wa kirafiki baada ya Everton kufanya hivyo mwaka 2017 chini ya udhamini wa Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa. Tunaizungumzia Sevilla iliyotwaa ubingwa wa Europa League mara tatu mfululizo chini ya Unai Emery.
Tunaizungumzia Sevilla yenye nyota kama vile Jesus Navas, Wissam Ben Yedder ambao wanapigana vikumbo na wachezaji nyota na bora duniani kama vile Lionel Messi, Benzema na wengine wengi.
Unapozungumzia Sevilla kuja Tanzania kucheza na bingwa wa nchi, ni zaidi ya mechi ya Simba na TP Mazembe au Al Ahly kwa sababu hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa bingwa wetu kuumana na klabu kutoka Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) kwenye ardhi yetu ya nyumbani.
USO KWA USO Tusubiri kuiona hiyo vuta nikuvute ya mfungaji bora wa ligi, Meddie Kagere dhidi ya beki shupavu kama Simon Kjaer ambaye almanusura aipeleke timu yake ya Taifa ya Denmark kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi. Tusubiri kuona pale katikati ya dimba jinsi James Kotei na Jonas Mkude watakavyomdhibiti Pablo Sarabia ambaye ametengeneza mabao 17 mpaka sasa kwenye msimu huu
Maneno MAZITO ya Shigongo, DC GONDWE na Sam Sasali Campus Night
The post SportPesa Imeleta Msisimko wa Soka Ujio wa Sevilla appeared first on Global Publishers.
0 Comments