Windows

Simba yangojea vigogo 29 Afrika


Wakati Simba ikiungana na timu nyingine 38 kutoka mataifa tofauti barani Afrika kujihakikishia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, zimebaki timu 29 ili kutimiza idadi ya jumla ya timu ambazo zitashiriki kwenye mashindano hayo msimu wa ujao wa 2019/2020.


Simba ilikata rasmi tiketi ya kucheza kwa mara ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida United, Jumanne iliyopita na kufikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.


Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao yatashirikisha timu 68 na hadi sasa timu 39 zimeshakata tiketi ya kushiriki, baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwenye nchi zao au kushika nafasi ya pili kwa zile nchi ambazo zinaingiza timu mbili kwenye mashindano hayo.


Timu hizo 29 ambazo bado zitaungana na zile 39 ambazo zimeshakata tiketi, zinatoka katika nchi 26 na pindi idadi ikitimia, baadhi zitaanza kucheza raundi ya awali, kisha raundi ya kwanza na baada ya hapo timu 16 za mwisho zitatinga hatua ya makundi ya mashindano hayo.


Ukiondoa Simba, timu nyingine 38 ambazo zimejihakikishia kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao ni Wydad Casablanca na Raja Casablanca (Morocco0, Al-Ahly (Misri), TP Mazembe na AS Vita (DR Congo), USM Alger na JS Kabylie (Algeria), Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates (Afrika Kusini), Green Eagles na Zesco united (Zambia), 1º de Agosto na Petro de Luanda (Angola), Horoya (Guinea), SO de l'Armée na FC San Pédro (Ivory Coast), UD Songo (Msumbiji), AS Otôho (Congo), KCCA (Uganda) na Rayon Sports (Rwanda).


Nyingine ni Green Mamba (Eswatini), Township Rollers (Botswana), Gor Mahia (Kenya), ASC Kara (Togo), FC Platinum (Zimbabwe), Rahimo (Burkina Faso), Aigle Noir (Burundi), AS Port (Djibout), Matlama (Lesotho), Big Bullets (Malawi), FC Nouadhbou (Mauritania), Pamplemousses (Mauritius), Black Africa (Namibia), JS Saint-Pierroise (Reunion), UDRA (Sao Tome and Principle), Génération Foot (Senegal), Côte d'Or (Shelisheli) na KMKM

Post a Comment

0 Comments