Windows

Kagere ataka rekodi nyingine

MSHAMBULIAJI Meddie Kagere wa Simba ametamba kutengeneza rekodi nyingine iwapo ataendelea kusalia katika kikosi cha Simba.

Kagere amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha Simba baada ya kuifungia timu hiyo mabao 23, licha ya kwamba ni msimu wake wa kwanza.

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya mchezo wao dhidi ya Biashara Utd kumalizika, alisema huwa anapenda kuvunja rekodi yake na sio rekodi ya mtu mwingine.

"Mimi napenda kuvunja rekodi yangu tu na sio rekodi ya mtu mwingine yoyote, kwahiyo kama hivi sasa nimefunga magoli haya basi msimu ujao nataka yaongezeke," alisema.

Aliongeza ubingwa wa msimu huu anaupeleka kwa mashabiki na benchi zima la ufundi pamoja na wachezaji wenzake kutokana na wote walijitoa katika kuhakikisha timu inafanya vizuri.
Straika huyo mbali na kuifungia Simba mabao 23 katika Ligi, pia ametupia mengine 15 katika michezo mbalimbali ikiwamo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la FA, Kombe la Mapinduzi, SportPesa na mechi za kirafiki kuonyesha alivyo mhimili wa Simba kwa sasa.


Post a Comment

0 Comments