Windows

SIMBA SC YALA KIPORO CHA TANZANIA PRISON KIBABE , YAIGONGA GOLI 1-0 NA KUCHUKUA POINTI ZOTE TATU

2 

Wachezaji wa timu ya Simba SC Haruna Niyonzima na Zana Coulibaly wakiwania mpira na mchezaji wa timu yaTanzania  Prison FC ya Mbeya katika mchezo wa Ligi kuu ya Tanzania (TPL) uliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo , Katika mchezo huo Simba SC Imeubuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Prison ikifikisha pointi 78 na kuikaribia  Yanga  inayongoza ligi ya TPL  kwa pointi 80, Goli la Simba SC limefungwa na Mshambuliaji wake kutoka Uganda Emmanuel Okwi.

4

Mchezaji wa timu ya Simba Meddy Kagere akikabiliana na wachezaji wa timu ya Prison ya Mbeya wakati mchezo katika ya Simba SC ya Dar es salaam  na Tanzania Prison FC ya Mbeya zikichuana kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo.

5

Mchezaji Hassan Dilunga wa timu ya Simba akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Tanzania Prison FC ya Mbeya wakati timu hizo zilipokutana katika mchezao wa Ligi Kuu ya Tanzania (TPL) leo kwenye uwanja wa mpira wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

3

Kocha wa viungo wa timu ya Simba SC Adel Zrane akiwafua wachezaji wa akiba wa Simba SC kabla ya kufanya mabadiliko na kuingia uwanjani.

6

Picha mbalimbali zikionyesha mashabiki wa Simba mkoani Mbeya waripuka kwa shangwe mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prison  lililofungwa na mshambuliaji wake Emmanuel Okwi.

7 8 9 10 11


Post a Comment

0 Comments