Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wako mkoani Singida ambapo leo watashuka katika uwanja wa Namfua kuikabili Singida United katika mchezo ambao huenda wababe hao wa soka la Tanzania watatawazwa mabingwa
Simba inayoongoza ligi ikiwa na alama 88, inahitaji alama moja tu katika mchezo huo ili iweze kurudi na kombe jijini Dar es salaam
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wataingia katika mchezo huo kusaka ushindi ingawa wanafahamu pointi moja itatosha kutimiza lengo la kutwaa ubingwa
"Tuko hapa kwa ajili ya kusaka ushindi, Nawakaribisha mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani kutuunga mkono ili tuweze kutimiza lengo la kutwaa ubingwa leo," amesema Aussemscut
Licha ya kukabiliwa na changamoto ya ratiba ya kucheza mfululizo, Simba inaelekea kutimiza azma yake ya kutwaa ubingwa
Ilicheza na Ndanda Fc juzi na jana asubuhi ikaondoka jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege mpaka mkoani Dodoma ambako ilichukua usafiri wa basi mpaka Singida
Baada ya mchezo leo Simba itarejea Dodoma na kesho asubuhi kuwahi jijini Dar es salaam ambapo keshokutwa inakabiliwa na mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla inayoshiriki ligi kuu ya Hispania, La Liga
Sevilla inatarajiwa kuwasili leo
Mchezo dhidi ya Sevilla nao una umuhimu wa kipekee kwa wachezaji kwani watapata nafasi ya kuonekana dunia kwani mchezo huo utaonyeshwa na vituo vya televisheni zaidi ya 56 kote duniani
0 Comments