Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia amekoshwa na ujio wa Sevilla akidai ni chachu ya maendeleo ya soka nchini.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo, Karia alisema kuwa uwepo wa mechi ya kirafiki baina ya Sevilla na Simba pamoja na shughuli nyingine ambazo watafanya ni vitu vinavyohamasisha maendeleo ya mpira wa miguu.
"TFF ina ushirikiano wa miaka mitatu na La Liga hivyo ujio wa Sevilla kuja kucheza na Simba ni ishara ya ushirikiano wetu ni mkubwa.
Mbali na mechi, pia kuna kliniki ya soka ambayo tunaiona ni fursa ya kuendeleza mpira wa miguu, lakini pia kutimiza sehemu ya makubaliano ya mkataba wetu na La Liga," alisema Karia.
Naye mkurugenzi wa maendeleo ya michezo, Yusuph Singo aliwahakikishia Sevilla usalama na ulinzi katika ziara yao nchini.
"Kwa niaba ya serikali ningependa kuipongeza SportPesa kwa kusaidia maendeleo ya michezo Tanzania. Kwa mara ya pili inaleta timu kubwa Tanzania. Ukiondoa michezo pia imekuwa ikitoa msaada wa mtu mmojammoja mfano kuendesha kliniki ya vipaji.
Kwa niaba ya serikali niwahakikishie usalama katika maeneo yote mtakayopita. Tanzania ni nchi yenye mashabiki vichaa wa soka na naamini mtafurahia.
“Nitoe wito kwa mashabiki kutumia fursa hii kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo. Wenzetu wanatoa hela nyingi kuwatazama lakini huku SportPesa wamewaletea kwa bei rahisi," alisema Singo.

0 Comments