Windows

Okwi, Kagere kuongoza vita ya kuinyatia Yanga leo



Timu ya Simba imeanika kikosi chake kinachoivaa Coastal Union ya Tanga leo Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


Kwenye kikosi hicho wapo Aishi Manura, Nicholas Gyan, Mohamed Hussein, Yusufu Mlipili, Erasto Nyoni, Said Ndemla, Clatous Chama, Jonas Mkude, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Rashid Juma ambao ndio watakaoanza.


Pia wachezaji wa akiba; Deogratus Munish Dida, James Kotei, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Mohamed Ibrahim, Adam Salamba na John Bocco.


Wakati Simba ikihitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kukalia usukani kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema timu yake haiwezi kuwa ngazi ya kuwapandisha mabingwa hao watetezi.


Simba yenye pointi 78 itapepetana na Coastal kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam mchezo ambao kama itashinda itaongoza ligi kwa kuwa itakuwa imefikisha pointi 81 na kuishusha Yanga inayoongoza kwa pointi 80.


Pia Yanga ina nafasi ya kurejea kileleni endapo itashinda mechi yake dhidi ya Biashara United iliyopangwa kuchezwa kesho mkoani Mara. Yanga ikishinda itafikisha pointi 83.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Mgunda alisema wamejiandaa vyema kupata pointi tatu katika mchezo huo. Alisema wachezaji wake wanatambua umuhimu wa mchezo huo na kila mmoja amejipanga kucheza kwa nguvu ili kupata matokeo mazuri na hawezi kuwa ngazi kwa Simba kupanda katika msimamo wa Ligi Kuu.


“Tunahitaji pointi tujiweke katika mazingira ya kumaliza ligi katika nafasi nzuri, lakini wenzetu pia wanasaka ubingwa na kukaa kileleni kwenye msimamo,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Taifa Stars.


Akizungumzia maandalizi ya timu yake, Mgunda alisema hawana hofu na mechi hiyo na wamejipanga kutoa ushindani ingawa anatambua mechi itakuwa ngumu kutokana na ubora wa Simba.


Post a Comment

0 Comments