Windows

Mwinyi Zahera kigeugeu

Katika kauli mbalimbali ambazo Kocha wa Yanga, Mkongo Mwinyi Zahera amekuwa akizoa kuhusiana na malengo ya kikosi chake kama zinapingana.

Kati ya zote iliyo kali zaidi ni ile aliyoitoa baada ya kikosi chake kung'olewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali na Lipuli FC ya Iringa ambayo itacheza fainali na Azam FC.
Zahera alisikika akisema, hawakuwa na mipango ya kuchukua kombe lolote msimu huu si Ligi Kuu wala Kombe la Shirikisho.

Amesema, kwenye ligi mipango ilikuwa ni kutomaliza nafasi juu ya 10 na wamalize na nafasi ya sita au saba kutokana na hali ngumu ya kikosi hicho. Hali ngumu na madai kuwa Yanga hawana pesa na wakafikia hatua ya kupitisha bakuri wakijichangisha.

"Malengo ya kubeba Kombe la FA yalikuja hapa katikati baada ya kuona tunafanya vizuri na tukakubaliana kuwa tunaweza hivyo tufanye kazi lakini kabla tulisema endapo Mungu akisaidia tumalize katika moja ya nafasi hizo mbili lakini mwisho wa siku ilikuwa hivyo,"alisema Zahera.

Amesema, hata hivyo kwenye Ligi Kuu hawajakata tamaa kwa kuhakikisha wanashinda mechi zao zilizobaki.

"Tumebakiwa na michezo minne sisi tunataka tushinde yote halafu mwisho wa siku tutajua kinachoendelea,"alisisitiza Zahera ambaye aliipokea Yanga ikiwa katika hali hiyo ngumu kiuchumi na kwa kipindi alichofanya kazi ni kama amefanikiwa.



Post a Comment

0 Comments