HATIMAYE Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Yanga iliyo chini ya mwenyekiti wake, Dk Mshindo Msolla, inakutana leo Jumamosi kupendekeza majina ya wajumbe watakaounda kamati ya usajili ya klabu hiyo huku aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, Hussein Nyika akiondolewa mazima.
Uongozi mpya wa Klabu ya Yanga umeingia madarakani Mei 5 ambapo upo katika mchakato wa kuimarisha kamati ya utendaji ili kuleta ushindani msimu ujao. Moja ya kazi ambazo wameamua kuanza nazo ni kuhakikisha wanakuwa na kamati imara ya usajili ambayo itaanza mchakato wa kufanya usajili mara moja baada ya kuteuliwa.
Taarifa ambayo Championi Jumamosi imezipata kutoka ndani ya Yanga, zinasema kuwa kamati ya utendaji ya klabu hiyo inatarajia kukutana leo kufanya uteuzi wa majina 10 ya kamati ya usajili itakayofanya kazi mara moja.
“Kamati ya Utendaji ya Yanga itakutana siku ya Jumamosi saa nne asubuhi katika klabu hiyo iliyopo katika mtaa wa Jangwani ili kuweza kutoa mapendekezo ya majina 10 ya kamati ya usajili ambayo itakuwa na jukumu la kufanya usajili mara moja ambayo itatangazwa wakati wowote kuanzia sasa.
“Kuna wajumbe mbalimbali ambao wameteuliwa kwa ajili ya kufanya kazi hiyo lakini wale waliopita akiwemo Nyika wajumbe wengi wamemkataa asiwemo katika kamati hiyo nyeti ndani ya klabu,” alisema mtoa taarifa huyo.
Aidha Championi lilimtafuta Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela ili aweze kuzungumzia juu ya kamati hiyo, alisema kuwa, mchakato bado unaendelea na mambo yakikamilika kila kitu kitawekwa wazi.
Mbwana Samatta Atumike Kwa Hili | Tembo wameshaua…
The post Nyika kachinjwa Yanga, 10 wapya kuunda kamati appeared first on Global Publishers.
0 Comments