

KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima, amesema kuwa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wazi kwa upande wao lakini kama watazubaa itakula kwao.
Akizungumza na BINGWA, Niyonzima alisema kuwa hivi sasa mechi zao zimekuwa na presha kubwa kwa kuwa tayari kunadhana ya kubwebwa inaenezwa vichwani mwa watu.
“Tunanafasi kubwa ya kuwa mabingwa msimu huu, lakini kwa kuwa tayari kunadhana mbaya juu yetu inaenezwa kama tusipokuwa makini tunaweza kutoka patupu.
“Kila mechi tunayopata ushindi lazima wapinzani wetu walalamike kwa kudai waamuzi wanatupendelea hiki kitu ni kibaya na kinaweza kutuvurugia malengo.
“Kwa michezo yetu mitatu tuliocheza unaona kabisa hakuna suala la kupendelewa kama inavyodaiwa, lakini ninachojua yanasemwa hayo ili kuwapa hofu waamuzi wanaotuchezesha na kuwajenga wapinzani tunaokutana nao kuwa Simba ni timu ya kupendelewa hivyo hawawezi kushinda.”alisema.
Niyonzima aliongeza: “ Kulingana na hali ilivyo lazima wachezaji, benchi la ufundi na viongozi tuwe makini kwa kuhakikisha tunakwepa hujuma zote zinazoandaliwa dhidi yetu ili kutimiza malengo ya ubingwa tuliyo nayo.”
Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Wekundu wa Msimbazi walikuwa na pointi 78 walizozipata katika michezo 30 waliocheza nyuma ya Yanga wenye alama 80 baada ya kushuka dimbani mara 34.
The post Niyonzima: Tukizubaa imekula kwetu appeared first on KWATA UNIT SPORTS & ENTERTAINMENT.



0 Comments