

Kiungo Haruna Niyonzima ameweka rekodi ya kipekee kwa kutwaa mataji matano mfululizo ya ligi kuu ya Tanzania Bara
Niyonzima aliyetua Simba miaka miwili iliyopita, jana alishinda taji lake la pili akiwa na Simba
Kabla ya kutua Simba, Niyonzima alishinda taji la ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo akiwa na Yanga
"Ubingwa wa tano mfululizo ndani ya ligi kuu Tanzania. Huu ndio mwanzo wa safari yetu, ndoto yangu ni kushinda mataji mengi zaidi na ubingwa wa Afrika nikiwa na kablu hii kubwa," amesema Niyonzima
Naye mshambuliaji Emmanuel Okwi ameingia katika vitabu vya Historia vya Simba baada ya kushinda mataji manne ya ligi kuu
Okwi ameshinda ubingwa wa ligi kuu akiwa na Simba misimu ya 2009/10, 2011/12, 2017/18 na 2018/19
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo kutoka mkoani Singida ambako kilitetea ubingwa janacut
Tayari timu iko Dodoma ambapo leo Jumatano itaondoka kwa usafiri wa ndege kurejea Dar kuwahi mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla utakaopigwa kesho uwanja wa Taifa
Simba inatarajiwa kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa sita mchana
Mashabiki wa Simba wametakiwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Ndege wa Kimataifa, JNIA kuwalaki mashujaa wao



0 Comments