Windows

Majembe yanayomaliza mikataba Yanga



Yanga iko katika mchakato wa kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao huku ikiwa na idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu

Ikiwa mbioni kumuuza msambuliaji wake Heritier Makambo, TP Mazembe inatarajiwa kumsajili kiungo Ibrahim Ajib ambaye nae mkataba wake uko mwishoni

Wakati mauzo ya Makambo yatainufaisha Yanga, kwa Ajib Yanga haitapata kitu kwani mchezaji huyo anaondoka akiwa huru

Yanga itapaswa kufanya uamuzi ya haraka juu ya baadhi ya wachezaji ambao mikataba inaisha la sivyo inaweza kuwapoteza wakiwa huru kama kilichotokea kwa Ajib

Aidha uongozi wa Yanga umeshauri kuanzisha utaratibu wa kuhuisha mikataba ya wachezaji kabla haijamalizika ili kuondokana na 'presha' ya usajili mwishoni mwa msimucut

Hawa hapa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika Yanga;

Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Pato Ngonyani (alitolewa kwa mkopo), Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma, Matheo Anthony na Mrisho Ngasa

wengine ni Thabani Kamusoko, Papy Tshishimbi, Raphael Daudi, Pius Buswita, Juma Mahadhi, Baruani Akilimali, Ibrahim Ajib (anaenda TP Mazembe), Amissi Tambwe na Haruna Moshi

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kabla hajasafiri kwenda Congo kujiunga na timu ya Taifa wiki ijayo, timu hiyo itakamilisha usajili wa wachezaji wapya nane

Bila shaka pia itakuwa imemalizana na wachezaji waliopendekezwa kuendelea kubaki Jangwani

Post a Comment

0 Comments