

Winga wa Yanga Mrisho Ngasa ametoa shukrani kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaunga mkono tangu mwanzoni mwa msimu licha ya changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili
Aidha, Ngasa amewapongeza viongozi wa Yanga waliokuwepo katika kipindi ambacho timu hiyo ilikuwa na matatizo na walifanikiwa kuyatatua kadiri ya uwezo wao
Amesema msimu ulikuwa mgumu sana kwao lakini kumaliza nafasi ya pili ni mafanikio makubwa kwa kuzingatia changamoto zilizokuwa zikiwakabili
Ngasa ameongeza kuwa kocha Mwinyi zahera alikuwa msaada mkubwa kwao kwani ilifika wakati aliwapa msaada wa fedha pale walipokwama
"Asante kwa wote mliokuwa pamoja nasisi katika kipindi kigumu mpaka kuweza kufika Hapa nijambo kubwa sana kumaliza nafasi ya pili," amesema
"Nawapongeza viongozi waliokuwepo kipindi cha matatizo na kuyatatuwa pia niwape Hongera mashabiki wote wa yanga Hakika meonyesha mchango mkubwa sana kwetu"
"Na pia nampongeza kocha mbali yakuwa kocha umesaidia pakubwa palipokwama kama nauli za watu umekuwa mtu wakutoa chako"
"Napongeza timu nzima Enjoy soccer kila Jema inshallah"cut
Ngasa ni miongoni mwa wachezaji ambao wanamaliza mikataba ya kuitumikia Yanga
Hata hivyo anapigiwa chapuo aongezewe mkataba mwingine kwani ukizungumzia wachezaji walioin'garisha Yanga msimu huu licha kukabiliwa na changamoto nyingi, Ngasa ni mmoja wao
Mkongwe huyo anaamini bado anao uwezo wa kuipa mafanikio Yanga siku za usoni
Licha ya usajili wake kubezwa, msimu uliomalizika amedhirisha bado mpira upo mguuni akifanikiwa kuifungia Yanga mabao manne



0 Comments