Windows

Nakuja kuwafurahisha mashabiki wa Yanga - Birigimana



Winga mpya wa Yanga Issa Birigimana 'Walcott' amesema baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria, anakuja nchini kufanya kazi

Birigimana anayemudu kucheza namba saba na namba tisa, amesema alikuwa na msimu mzuri katika klabu ya APR, anaamini atahamishia makali hayo ligi kuu ya Tanzania Bara

"Nimesaini Yanga miaka miwili, nakuja kuwafurahisha mashabiki wa Yanga Tanzania," amesema

Bigirimana ataungana na kiungo fundi Patrick Sibomana ambaye nae ametokea klabu ya Mukura Victory ya hukohuko Rwanda

Nyota hao wamesajiliwa baada kuidhinishwa na kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera

Post a Comment

0 Comments